November 23, 2024, 3:20 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI KUFUNGUA BUNGE NOV 10, 2020
Rais Dkt. John Magufuli anatarajiwa kufungua Bunge la 12 Novemba 10, 2020 baada ya wananchi kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua wabunge watakaowawakilisha kwa kipindi cha miaka mitano.
Taarifa iliyotolewa hii leo Novemba 7, 2020 na Katibu wa Bunge imeeleza kuwa siku hiyo shughuli mbalimbali zitafanyika ambazo ni pamoja na kusomwa kwa tangazo la Rais la kuitisha Bunge, uchaguzi wa spika na naibu spika, kuthibitishwa kwa uteuzi wa waziri mkuu.
Shughuli nyingine ni kiapo cha uaminifu kwa wabunge wote.
Wabunge wateule wametakiwa kwenda na nyaraka mbalimbali ikiwemo hati ya kuchaguliwa/kuteuliwa kuwa mbunge, nakala ya kitambulisho cha Taifa na vyeti vya elimu.