- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI ASEMA BUNGE LA NDUGAI LILIKUWA LA KISASA
Rais wa TANZANIA, Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI leo tarehe 16 Juni, 2020 analihutubia na kulifunga Rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA.
Katika hafla hiyo inayofanyika leo Bungeni imehudhuriwa na viongozi wengi Miongoni mwa waliohurudhia Bungeni hapa ni pamoja na Marais Wastaafu wote pamoja na mawaziri wakuu wastaafu wote, Mkurugenzi Mkuu wa usalama wa Taifa na wengine.
Rais MAGUFULI amesema ameshuhudia mabadiliko mengi makubwa Bungeni tofauti na wakati alivyokuwa Mbunge na amewapongeza Wabunge kwa kulifanya Bunge hilo kuwa la kisasa.
Amesema kwa miaka mitano iliyopita, wameweza wametekeleza wajibu wao na kuwatumikia Watanzania. Pia amewashukuru MARAIS waliomtangulia kwa kumuwekea misingi imara
Aidha, Rais MAGUFULI amewashukuru Madiwani kwa kutekeleza shughuli mbalimbali katika maeneo yao huku akisema viongozi hao ni kiungo muhimu kati ya Serikali na Wananchi
Rais MAGUFULI pia ameeleza kuwa, mojawapo ya ahadi aliyoitoa ni kudumisha amani na muungano na ZANZIBAR na kuliambia Bunge kuwa ahadi hiyo imetimizwa kwa vitendo na Watanzania wameendelea kushikamana.