Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 4:56 pm

NEWS: RAIS MAGUFULI AMTUMBUA WAZIRI ALIYEFUTA VYETI VYA UWALIMU


Rais John Magufuli ametengua UTEUZI wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt Ave Maria Semakafu.

Utenguzi huu unakuja muda mchache baada ya Naibu huyo kutangaza Kufuta mtaala wa ualimu wa ngazi ya cheti kwa elimu ya awali na msingi.

Akizungumza Jana jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo Dk Ave Maria Semakafu alisema hatua hiyo inakwenda sambamba na kufanyia kazi maoni ya wadau ambao wamekuwa wakiyatoa likiwemo kufuta mtaala huo.

“Mtaala ulioboreshwa unatoa nafasi kwa mwalimu katika mwaka wa pili wa masomo kuchagua eneo la umahiri atakalobobea tofauti na mfumo wa zamani ambao haukuwa katika muktadha huo,” amesema.

Alisema mtaala huo mpya utaanza kutumika katika mwaka wa masomo 2020/2012 na kwamba mwalimu yeyote mwenye cheti cha ualimu atakuwa na sifa ya kusomea Diploma ya Ualimu wa Elimu ya Awali au Msingi na vile vile atakapohitimu na kufaulu atakuwa na sifa ya kujiunga na Chuo Kikuu kupata Shahada ya Kwanza ya Ualimu kwa elimu ya awali au msingi.

“Programu itakayofundishwa itakuwa ya miaka mitatu na masomo yatafundishwa kwa lugha mbili ambazo ni Kingereza na Kiswahili kutokana na kuwepo kwa shule za English Medium nchini,” amesema.

Alisema waliosoma Astashahada (cheti) bado serikali inatambua uhitimu wa cheti katika kada ya ualimu na ipo kwenye mfumo wa utumishi na itaendelea kuwepo na hakuna mwalimu atakayefukuzwa kazi kwa kuwa yeye ni mwalimu wa ngazi ya cheti.