- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AMFUTA KAZI MKUU WA MKOA WA ARUSHA
Rais John Pombe Magufuli ametengeua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na nafasi yake kuchukuliwa na Idd Kimanta aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli.
Aidha sambamba na hilo Rais ametengeua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya ArushaGabriel Daqarro na Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo alikuwa na mvutano wa kiutendaji na Mkuu wa wilaya yake Bw Gabriel Daqarro.
Ipo video inayosambaa mitandaoni ikionesha wawili hao wakirushiana maneno Juu ya ubora wa mabati yaliyotumika katika ujenzi,
Mkuu wa Mkoa bwana Mrisho Gambo alionekana akimtuhumu "uongo" mkuu wa Wilaya bwana Daqaro,. Na kudhihirisha kuwa ulikuwa ni uongo, mkuu wa Wilaya huyo hakumwacha Mkuu wa Mkoa andelee kupotosha akamsahihisha palepale RC Gambo baada ya hapo akaendelea kutoa shutuma.