Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 8:43 pm

NEWS: RAIS MAGUFULI AMETAHADHARISHA KUHUSU CHANJO YA CORONA

(Muakilishi) Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametahadharisha vikali kuhusu chanjo inayotolewa na wataalamu wa afya ya Covid 19 ambayo chanjo hiyo imeanza kutolewa katika mataifa mbalimbali duniani hasa nchi karibu zote za Ulaya.

Rais Magufuli ameendelea kuweka wazi msimamo wake juu ya Ugonjwa wa Corona, huku akionyesha kukerwa vikali na wale waliokimbilia nchi za nje ili kupata chanjo hiyo ambapo amewashutumu kwa kuleta Corona ya ajabu ajabu

‘’tusiwe tunakimbilia masuala chanjo chanjo, si kila chanjo ina faida kwetu, ni lazima Watanzania tuwe macho, tuwe waangalifu, tutafanyiwa majaribio.”

Kauli hiyo Rais Magufuli ameitoa hii leo Januari 27, 2021 na kiwataka watanzania kuchukua tahadhari kwa kujifukiza na kuendelea na maombi.

‘’Tutaendelea kuchukua tahadhari, pamoja na kujifukiza, kusali na kuswali, huku tukiendelea na shughuli zetu, ule vizuri ushibe corona ashindwe kuingia kwenye mwili wako’’.

Msimamo wa Rais Magufuli unaachana na msimamo wa Baraza La maaskofu wa kanisa katoliki ambao unaoonesha kutambua uwepo wa corona na kuwataka waumini na wananchi kuwa na tahadhari Juu ya ugonjwa huo.