- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AFUTA USHURU SOKO LA URAFIKI
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM na Rais wa Tanzania John Magufuli amefuta Ushuru katika Soko la Urafiki maarufu ' Mahakama ya Ndizi' na badala yake amewataka kununua vitambulisho vya machinga kwa thamani ya shilingi elf 20 kwa mwaka.
Aidha Rais Magufuli amekabidhi Soko hilo kuanzia sasa kuwa chini ya wananchi.
Awali eneo hilo la Soko lilikua likimilikiwa na Kiwanda cha Urafiki chama hapa jijini Dar es salaam.
Uwamuzi huo wa Rais Magufuli ameutoa hii leo Octoba 13, 2020 wakati wa mkutano wake wa kampeni alioufanya katika eneo la Mburahati Jijini Dar es salaam.
"Kuna matatizo gani kwenye mahakama ya ndizi?, Kwa mamlaka niliyonayo kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mahakama ya ndizi itabaki chini ya wananchi wa hapo wanaofanya biashara, wanaofanya biashara kwenye mahakama ya ndizi hakuna kulipa ushuru watalipia vitambulisho tu, mmenifurahisha mno ninaweza nikatoa ahadi zingine ambazo nitashindwa kuzitekeleza" Ndg. John Pombe Magufuli - Mgombea Urais Kupitia CCM.
"Kwa mamlaka niliyonayo kama Rais, kama kuna taratibu zingine za sheria ya ardhi namba nne na tano ya mwaka 1996 na ile ya 2007, kuanzia leo hakuna kulipa ushuru, mtalipia kitambulisho tu," amesema Magufuli katika Kampeni zake uwanja wa Barafu Mburahati hii leo.