Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 4:54 pm

NEWS: RAIS MAGUFULI AELEZA ALIVYOAMUA KUANZA KUJENGA UCHUMI

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dk.John Magufuli ameeleza kuwa katika nchi yoyote ukitaka kujenga uchumi ni lazima uanze na vitu vinavyochochea uchumi, huwezi kutaka kujenga uchumi wakati vitu vinavyochochea uchumi havijaendelezwa,

Dk.Magufuli amesema hayo leo Septemba 4, 2020 mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni za kuomba kura kuelekea uchaguzi mkuu unaotatarajia kufanyika Oktoba 28, 2020.

“Hata Mungu mwenye alipotaka kuiumba Dunia hakuanza na watu, alianza na ardhi ili watu waje waitumie kulima,akaleta jua ,a akaleta dunia baadae akaleta wanyama na ndege ili binadamu watakapokwenda katika ardhi ile wakaitawale na alitumia siku sita na ya saba akampumzika,”amesema Dk.Magufuli

Hata hivyo amefafanua mbele ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu kwamba alipoingia madarakani aliona atumie mbinu ya kujenga uchumi wa kisasa katika nchi hii na ndio maana walianza na miundombinu na anakumbuka hata Bariadi watu walikuwa wanakufa bila kutibiwa hospitali na walikuwa wanabebwa kwenye tela za ng’ombe.

“Mmesahau, tukasema lazima tujenge hospitali kubwa ya Rufaa itakayofanya upasuaji wa aina zote, wakati nakwenda kuweka jiwe la msingi watu hawakuwamini kama kutakuwa na hospitali ya rufaa , leo pale Itilima, leo haa Bariadi hospitali ipo,

Wakati anaingia madarakani hii barabara haikuwepo na anakumbuka wakati anabomoa nyumba zilizokuwepo kwenye hifadhi ya barabara alisema ipo siku moja watu wa Simiyu watafurahi.”Tumejenga miundombinu ya barabara ili kutengeneza uchumi wa kisasa”.

Akizungumza zaidi na wananchi wa Simiyu amewaahidi kwamba wakimchagua tena miaka mitano mingine atahakikisha ndani ya miaka mitatu vijiji vyote kijiji kitakuwa na umeme kwani tayari vijiji zaidi ya 10,000 tayari vina umeme na vibaki vijiji 2600.

“Nataka kusema hili Simiyu, sitaki kusema mbele ya Mungu, mkitupa miaka mingine mitano nina uhakika kama mitatu vijiji vyote vitakuwa na umeme, ndio maana nakuja kuwaomba kwanini watu wafanye majaribio hatawatufikisha mahali.

“Tumehangaika wote, tumebana mafisadi wote, tumeanza viruzi, ndio maana nafikiri watu wa Bariadi na Simiyu mnipe kura ili tuendelee,”amesema Dk.Magufuli wakati anazungumza na wananchi hao