Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 1:37 pm

NEWS: RAIS MACRON AKOSA WINGI WA VITI BUNGENI

Ufaransa(MuakilishiTZ). Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na washirika wake Jana Jumapili Juni 19, 2022 hawamekosa wingi wa viti vya bunge kwenye duru ya pili ya uchaguzi na hivo kutoweza kudhibiti ajenda yake ya mageuzi. Hili ni pigo kubwa kwa rais huyo aliyechaguliwa kwa muhula mwingine hivi karibuni.

Bila shaka, muungano wake wa mrengo wa kati Ensemble ulitarajia kupata viti vingi katika uchaguzi wa Jumapili, ukifuatiwa na muungano wa mrengo wa kushoto Nupes unaongozwa na mwanasiasa mkongwe mwenye siasa kali za mrengo wa kushoto Jean Luc Melenchon, makadirio ya awali yameonyesha.

Lakini Macron na washirika wake hawatapata wabunge wa kutosha wanaohitajika kudhibiti bunge, mawaziri na washauri wake wa karibu wamekiri, wakisema watalazimika kushirikiana na vyama vingine mbali na muungano wao ili kuingoza nchi.

Waziri wa fedha Bruno Le Maire ameyataja matokeo ya uchaguzi kuwa "msisimko wa kidemokrasia" na kusema watashirikiana na vyama vyote vinavyounga mkono Umoja wa Ulaya kusaidia kuiongoza nchi.

Ikiwa matokeo hayo yatathibitishwa, bunge litaanza kipindi cha siasa kisichokuwa na uhakika ambacho kitahitaji kushirikiana madaraka kati ya vyama ambavyo havina uzoefu nchini Ufaransa katika miongo ya hivi karibuni au kukwama kwa siasa hata uwezekano wa kufanya uchaguzi mwingine.

Makadirio ya taasisi za kura ya maoni Ifop, Opinion way na Ipsos yameonyesha muungano wa Macron Ensemble ukishinda kati ya viti 210 na 240, huku muungano wa Nupes ukipata kati ya viti 149 na 188.