- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS KENYATTA AONGEZA MARUFUKU YA KUTOTOKA NJEE KWA SIKU 30
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza hatua ya kuongeza marufuku ya siku 30 ya kutotoka nje nchini humo, na shughuli za usafiri katika maeneo ya Nairobi na Mombasa zimesitishwa pia kwa muda huo.
Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi, Kenyatta ameondoa marufuku ya kutotoka nje katika maeneo ya Eastleig, na Old Town kuanzia saa kumi asubuhi tarehe 7, Juni, 2020.
Kaunti za kwale na Kilifi pia zinafunguliwa kuanzia saa kumi asubihi 7, Juni 2020 kwa sababu maambukizi yameanza kupungua katika maeneo hayo.
Wakati huohuo, rais amelegeza masharti ya kutotoka nje usiku ,hatua ya kusalia ndani sasa itaanza kuwanzia saa tatu usiku hadi kumi asubuhi.
Bwana Kenyatta amefafanua kuwa kama kulegeza masharti kwa asilimia 20 kungesababisha maambukizi laki 2 na vifo 30,000 kufikia Desemba.
" Ikiwa masharti yangelegezwa kwa asilimia 60, kilele chake kingefikia Oktoba na maambukizi 450,000 na vifo 45,000," rais amesema.
Rais ameelezea mifano ya nchi zingine kama Korea Kusini, Pakistan na Malaysia na kuweka bayana kwamba ukosefu wa mchakato makhususi wa kufungua tena shughuli maambukizi yanaweza kuongezeka zaidi au kupata wimbi la pili la maambukizi.
Kituo kilichotengwa cha Siaya kina vitanda kumi na tayari watu 9 wamelazwa. Kituo cha Busia kilichotengwa kuhudumia wagonjwa wa Covid-19 kina vitanda 34 na kituo hicho kilijaa wagonjwa siku mbili zilizopita. Kwa mifano hiyo ameeleza kuwa ikiwa hatua muafaka hazitachukuliwa kuna uwezekano mfumo wa huduma wa afya ukalemewa.
Tangazo lingine ni shule kufunguliwa kuanzia Septemba mosi.
Rais amedokeza kwamba haikuwa kazi rahisi hata kwa timu yake ya wataalamu juu ya suala la kufunga au kufungua uchumi wa nchi.
"Lazima tukubali kwamba sio suala la kuwa uko sahihi au hauko sahihi, tumejikuta katika yote mawili ambayo ni sawa. Wale wanaotaka kufungua uchumi wako sahihi na wale wanaopinga ufunguaji wa uchumi pia wako sahihi," amesema.
Rais ameelezea kwamba hata yeye ni furaha na nia yake kufungua uchumi wakati huu kama ilivyo kwa raia.
Rais ametaka watu kuwa wa kweli na hali jinsi ilivyo na kusisitiza kwamba ikiwa hatua zilizopo hazingechukuliwa hali ingekuwa mbaya zaidi.
"Lazima tuambiane ukweli. Kiwango cha maambukizi Kenya kingekuwa juu sana ikiwa si kwa hatua tulizochukua awali."