- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS ATAKA ASKARI WALIOPANDA VYEO KUENDELEA KUSIMAMIA WAFUNGWA
Dodoma. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameliagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha askari wake waliopanda vyeo kuendelea kutekeleza majukumu yao kama kawaida na kuacha tabia ya kurundikana ofisini pasipokuwa na kazi kwa kigezo cha kupanda cheo.
Samia ametoa maagizo hay leo Ijumaa Machi 25, 2022 katika uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi ya makao makuu ya Magereza Dodoma
“Haina maana kama mtu ana cheo akabaki ofisini hana kazi, na kama umepandishwa vyeo nina hakika kuna watu wanazurura kwenye korido za maofi hawana kazi, warudi wakasimamie wafungwa.
“Hatuwezi kuajiri kila mwaka. Msitulazimishe kuajiri watu wapya kwa sababu watu wengi wamepanda vyeo vinginevyo mtanifanya sasa nisipandishe kwa sababu nikipandisha mnakuwa hamna kazi ya kufanya” amesema Rais Samia