- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI YAMTKA ZITTO NA WENZAKE 7 KURIPOTI TENA MWEZI HUU
LINDI. Jeshi la Polisi Mkoani Lindi limemtaka Kiongozi Mkuu wa ACT wazalendo Zitto Zuberi Kabwe na wenzake saba kuripoti tena kituo cha Polisi cha Lindi Julai 20 mwaka huu, baada ya kufanya hivyo hii leo Julai 1, 2020 kama walivyoamriwa na Jeshi hilo.
Zitto na wanachama wengine 7 wa chama hicho wanatuhumiwa kwa kosa la kuhatarisha Amani hii ni baada ya kiongozi huyo kufanya kikao cha ndani Mjini Kilwa cha chama cha kujipanga na uchaguzi mkuu ujao.
"Dola inadhani inatudhibiti kwa usumbufu huu wa nenda rudi. La hasha, sisi tunatumia huo ‘usumbufu’ kujenga Chama chetu na kuunganisha Watanzania ili kuleta mabadiliko ya kisiasa yatakayoleteleza ubora wa Maisha yao" amesema Zitto Kabwe muda mfupi baada ya kutoka kuripoti kituo cha Polisi Kilwa.
Zitto alikamatwa siku ya Jumanne asubuhi tarehe 23 Juni 2020 akiwa anajiandaa kuongoza kikao cha ndani cha wanachama wa chama hicho. Kikao hicho, kilikuwa kilikuwa kinafanyikia ukumbi wa Stamford Bridge ulipo Kilwa Masoko. Mbali na Zitto, wengine wanao tuhumiwa ni Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleman Mbungara maarufu ‘Bwege’ na Sheweji Mketo ambaye ni Katibu wa Kamati ya Oganaizesheni ya chama hicho