Home | Terms & Conditions | Help

April 6, 2025, 7:09 pm

NEWS: POLISI UGANDA YAMZUIA BALOZI WA MAREKANI KUMUONA BOBI WINE

Uganda. Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Uganda jana vimemzuia Balozi wa Marekani nchini humo Natalie E. Brown kwenda kumtembelea nyumbani kwake kiongozi wa upinzani na mgombea Urais nchini Uganda Robert Kyagulani maarufu Bobi Wine.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ubalozi huo wa Marekani.

‘’Lengo la balozi Brown lilikuwa ni kuangalia afya na usalama wa Bobi Wine hasa ikizingatia kwamba hajaruhusiwa kutoka nyumbani tangu uchaguzi huku maafisa wa usalama wakiwa wamezingira nyumba yake" imesema sehemu ya taarifa.

Balozi huyo alikuwa anatekeleza jukumu lake ambapo Marekani mara kwa mara hukutana na wadau mbalimbali wa kisiasa nchini Uganda kama sehemu ya shughuli zake za kidiplomasia.

‘’Tunatoa wito kwa serikali ya Uganda kuheshimu haki za raia wake na uhuru wa msingi, ikiwemo uhuru wa kujieleza, uhuru wa kukusanyika na uhuru kwa vyombo vya habari kama ilivyo katika katiba ya Uganda na kulingana na kujitolea kwa Uganda kuendeleza haki za binadamu.’’

Ubalozi wa Marekani unasema hakuna yeyote anayestahili kunyimwa uhuru wa kuwasiliana na uhuru wa kuondoka nyumbani kwake anapotaka kufanya hivyo.