November 23, 2024, 5:26 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI GEITA WAKANUSHA KUPENDELEA ULINZI BAADHI YA VYAMA
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe amekanusha taarifa za kwamba kunaupendeleo wa ulinzi katika mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa na kupendelea baadhi ya vyama kwa kusema kuwa vyama vyote vinapewa ulinzi sawa bila upendeleo hata kama mkutano una watu wawili.
Kamanda Mwaibambe ameongezia kuwa wamekuwa wakitoa ulinzi sawa kwa vyama vyote huku akiwataka wagombea ubunge na udiwani kufanya kampeni kwa kufuata muda uliowekwa na tume ili kuepuka vurugu na kushambuliana kwa mawe.