- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ORODHA YA WATUMISHI WAPYA WALIOCHAGULIWA
Dodoma. Serikali imetangaza watumishi wapya 9,675 wa kada za elimu na afya walioajiriwa kufuatia kibali cha ajira kilichotolewa na Rais wa sasa wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan, mwezi Aprili, 2021.
Orodha ya Majina ya waliopangiwa vituo vya kazi yanapatikana katika tovuti ya ofisi ya Rais-Tamisemi ya www.tamisemi.go.tz. au bofya hapa Majina ya walimu
Bofya hapa kupata ORODHA YA WATUMISHI WA AJIRA MPYA KADA ZA AFYA
Watumishi hao wapya wametangazwa na katibu mkuu ofisi ya rais Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe.
Profesa Shemdoe ametangaza ajira za elimu 6,749 kwa shule za msingi na sekondari na wataalamu wa afya 2,726.
Amesema waombaji wa kada ya ualimu walikuwa 99,583 na wataalam 37,437 wa kada ya afya wakiwemo wenye ulemavu 1,099 waliomba nafasi hizo.
“Baada ya kukamilisha taratibu zote za uchakataji wa maombi walimu 6,949 (3,949 wa shule za msingi na 3,000 wa shule za sekondari) na wataalam wa kada za afya 2,726 wamepangiwa vituo vya kazi,” amesema Profesa Shemdoe
Amewataka waajiriwa wapya kuripoti kwa wakurugenzi na kufanya kazi kwenye vituo walivyopangiwa na sio katika makao makuu ya halmashauri.
ORODHA YA WALIMU WA AJIRA MPYA
Profesa Shemdoe amewataka waajiriwa wapya kuripoti katika vituo vyao vya kazi wakiwa na vyeti halisi vya kidato cha nne na sita, vyeti halisi vya kitaaluma vya kuhitimu mafunzo katika kada husika, kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho ya Nida pamoja na cheti halisi cha kuzaliwa.
Pia, amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri ambazo zimepangiwa waajiriwa wapya kuwapokea na kuwawezesha kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma na baadaye kutoa taarifa ya kuripoti kwao katika ofisi ya rais Tamisemi.