Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 9:08 am

NEWS: NYUMBA YA POLEPOLE YAVUNJWA MCHANA KWEUPE

Dodoma. Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limedhibitisha taarifa za kuvunjwa na kuibwa vitu vya ndani vya mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole nyumbani kwake kata ya Ipaga Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amesema ipo taarifa ya mbunge huyo kuripoti tukio hilo jana desemba 12 saa 3.30 usiku.

Polisi wanasema kuwa wezi hao wanaonesha kuvunja dirisha na kuingia ndani na kuiba Flat Tv aina ya Hisense inchi 55 na spika ya Bluetooth aina ya JBL Extreme ambavyo thamani yake haijafahamika.

"Taarifa zinaonyesha kuwa, Mheshimiwa Polepole alisafiri Novemba 29,2021 kwenda Manyara kikazi lakini jana aliporudi alikuta dirisha limevunjwa ma wezi kuchukua vitu hivyo," amesema Kamanda Lyanga.

Taarifa za kuibiwa kwa Polepole zilisambaa kuanzia jana usiku baada ya Mbunge huyo kuweka taarifa katika ukurasa wake kwenye mtandao.

Taarifa zisizo rasmi zilieleza kuwa Polisi wamefika mchana nyumbani kwa mbunge huyo lakini hawakumkuta na simu yake haikuwa hewani.

Kamanda Lyanga ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kuwa waangalifu wanaposafiri kuweka mali zao kwa uangalifu huku akiahidi kuwasaka wahusika popote walipo iki kuwatia mbaroni.