- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NI RASMI URUSI YAIVAMIA UKRAINE
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba ametangaza kuwa Urusi imeanzisha uvamizi kamili dhidi ya nchi yake. Hapo Awali Rais Vradimir Putin alisema jeshi la Urusi litafanya operesheni maalum tu ndani ya Ukraine kama kulinda amani, lakini kinachofanyika sasa ni Vita imeanza.
Katika ujumbe aliouchapisha ukurasa wake wa mtandao wa twitter, waziri Dmytro Kuleba amesema, ''Putin ameanzisha uvamizi kamilidhidi ya Ukraine. Miji yenye amani ya Ukraine inakabiliwa na mashambulizi.''
Waziri huyo ameongeza kuwa tukio hilo ni vita vya ukandamizaji, na kuapa kuwa Ukraine itajilinda na itashinda, na kuwakumbusha viongozi wa dunia kuwa wana wajibu na uwezo wa kumsimamisha Putin.
Picha za kamera za usalama zimeonyesha misafara ya magari ya kijeshi ya Urusi ikiingia kwenye ardhi ya Ukraine kutoka katika rasi ya Crimea iliyonyakuliwa na Urusi.
Jeshi la Urusi linahakikisha kwamba linalenga maeneo ya kijeshi ya Ukraine pekee. Moscow imedai kuharibu kambi za jeshi la wanaanga za Ukraine na mfumo wa ulinzi dhii ya mashambulizi ya anga, huku Kiev ikidai kudungua ndege tano za Urusi na helikopta moja.
► "Msiogope", "tutashinda", amesema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika hotuba yake kwa taifa. Ametangaza sheria ya kijeshi kote nchini.
► Mabalozi wa nchi 30 wanachama wa NATO wanatarajia kukutana haraka Alhamisi asubuhi huko Brussels.
► Ufaransa, kupitia rais wake Emmanuel Macron, imelaani vikali "uamuzi wa Urusi kuanzisha vita dhidi ya Ukraine". Rais wa Ufaransa aliitisha baraza la ulinzi saa tatu.