- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NEC YAWARUDISHA WAGOMBEA 15 WA UBUNGE
Dodoma. Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania NEC imetoa uamuzi wa rufaa 55 za Wagombea mbalimbali wa nafasi ya Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao, ambapo katika rufaa hizo rufaa 15 zimekubaliwa na wagombea kurejeshwa kwenye orodha ya wagombea.
Taarifa iliyotolewa hii leo Septemba 8, 2020 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt Wilson Mahera imeeleza kuwa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa zimekataliwa na rufaa nyingine 25 za kupinga walioteuliwa zimekataliwa.
NEC imesema imefikia uamuzi huo baada ya kupitia vielelezo, nyaraka na maelezo ya warufani na warufaniwa vilivyowasilishwa ili kuhakikisha haki inatendeka kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kuanzia leo na kuendelea, na kwamba tayari wahusika wa rufaa hizo wameanza kujulishwa kuhusu uamuzi huo.