- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NEC YATUPILIA MBALI PINGAMIZI MGOMBEA WA CCM JIMBO LA MUHAMBWE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe DIOCLES MUGISHAGWE imetupilia Mbali pingamizi la Mgombea wa CCM Dkt. Florence George Samizi dhidi ya Mgombea wa ACTwazalendo Julius Masabo baada ya kuona utetezi wa Pingamizi lake kukosa mashiko kulingana na Sheria ya taifa ya uchaguzi.
Mapingamizi hayo yaliyoletwa na Mgombea wa CCM yalikuwa yanadai kuwa mgombea wa ACT Wazalendo Ndugu Julius Masabo alikosea kuambatanisha picha nne zenye muonekano wa rangi nyeupe kwa nyuma huku pingamizi la pili likiwa ni kutokukidhi idadi ya wadhamini waliotakiwa.
Uchanguzi huo wa Jimbo la Muhambwe unatokana na Jimbo kubaki wazi kufatia kifo cha Mbunge ea jimbo hilo na alikuwa naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Atashasta Justus Nditiye, kufariki dunia Februari 12 mwaka huu.
Nditiye alikuwa mbunge wa pili kufariki katika Bunge la 12 baada ya Martha Umbulla, aliyekuwa mbunge wa viti maalum (CCM), kufariki hivi karibuni.
Tayari tume ya uchaguzi imekwishatoa ratiba ya uchaguzi huo mdogo ambapo fomu zitaanza kutolewa kwa wagombea kutoka vyama mbalimbali vya siasa Machi 28 hadi April 3 ambayo ndio siku ya uteuzi wa wagombea na kampeni zitaanza April nne hadi mei mosi.