- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NDOA YA LULU NA DJ MAJIZO IMEYEYUKA HEWANI
MCHUMBA wa Msanii wa kike wa Bongomovie Elizabeth Michael maarufu Kama Lulu, Francis Siza maarufu Dj Majizzo amempa hongera Mrembo huyo kwa uvumilivu wake kipindi chote tangu amvishe Pete mwanzo mwa mwaka huu 2019 na kuhudhuriwa na watu lukuki, huku zikiwa zimebakiwa siku kadhaa kumalizika kwa mwaka huu.
Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram wa Majizzo ameandika ujumbe kama ishara ya kuonyesha kumkubali Lulu.
"Nakukubali mshikaji wangu japo mwaka umeisha na ndoa haina dalili lakini bado hujanikatia tamaa nakukubali Sana,"
Aidha, Mrembo huyo wa tasnia ya Bongomovie hakusita kumjibu mchumba wake .
"Nakukubali bro, Mswahili Numero uno tushakuwa ndugu tena maana umenipiga password mpaka tumeanza kufanana yote kheri 2019 nimekosa wedding nimepata twin,"
Hata hivyo Majizzo amempongeza mwanadada Maua sama kwa kuingia jukwaani kwa aina yake akiwa juu ya chuma na kulitendea haki jukwaa la tamasha Muziki mnene lililofanyika wiki iliyopita katika viwanja vya Tanganyika Packers kawe jijini Dar es salaam.
"Waswahili tulikua na hofu kama umeweza kupanda kwenye stage ukiwa juu ya hilo chuma,haikuwa ngumu kwako ukatimiza majukumu yako.