- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NDALICHAKO ATOA MAAGIZO KWA WAAJIRI.
DODOMA: Waajiri wote nchini wameagizwa kuhakikisha wanafanya vikao vyote vya baraza la wafanyakazi kwa mujibu wa sheria iliyowekwa ili kuwasaidia kufikisha masuala yao na maslahi binafsi.
Akizungumza Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amesema mabaraza yanapoisha muda wake wa kufanyika kunakuwa na kuchelewa kuyaunda upya.
“Vyama vya wafanyakazi vimeonyesha kufurahishwa na hatua ambazo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akizichukua kushughulikia masuala ambayo yanahusu wafanyakazi kuhusiana na mabaraza ya wafanyakazi ni takwa kisheria nachukua fursa hii kuwaagiza waajili wote kuhakikisha mabaraa ya wafanyakazi yanafanyika kwa wakati kwa mujibu wa sheria,”amesema
Ameongeza kwa kusema waajiri wanatakiwa kutambua kuwa mabaraza ya wafanyakazini daraja kati ya waajiri na waajiliwa ambalo lengo ni kufikisha masuala yanayohusu wafanyakazi na maslahi binafsi.
Kuhusu watumishi kuwekwa ndani kwa makosa yasiyokuwa ya kijinai waziri Ndalichako amesema serikali imeshatoa miongozo kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya wasiweke watumishi ndani kwa makosa ambayo siyo ya jinai.
“Nachukua fursa hii kuwakumbusha wakuu wa mikoa na wilaya kutekeleza maelekezo ya serikali kwasababu wakati maelezo yanatolewa nilipewa nakala inayotoa maelekezo kwa wateule hao kuacha kuwaweka ndani watumishi kwenye masuala ambayo sio ya kijinai,”ameeleza
“Serikali inataka kuona kuwa watumishi wanafanya kazi kwa kuzingatia mujibu wa sheria na pale wanapokosewa wanaadhibiwa kwa mujibu wa sheria zilizowekwa za kushughulikia masuala ya utovu wa nidhamu mahali pa kazi,
Naye Rais wa TUCTA Tumain Nyamhokya amesema kikao hicho ni kikao kidogo cha kikatiba ambacho huwakinapisha bajeti ya shirikisho.
Alisema TUCTA inaahidi kuendelea kumpa ushirikiano Rais Samia na wanaamini katika sherehe za mei mosi za mwaka huu atafanya kitu kwa wafanyakazi,
“watumishi wa umma wanakilio kikubwa dhidi ya wakuu wa mikoa na wilaya kuwa na tabia ya kuwasweka lupango watumishi jambo ambalolimetusikitisha sana kila wilaya unayoenda unakutana na watumishi 10 u 20 wako ndani,”amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya wanawake Tucta Rehema Ludanga amesema wafanyakazi wanazidi kujenga imani kwa serikali yao kwa kushirikiana na vyama vya wafanyakazi katika changamoto mbalimbali.
Amesema serikali inaona na kutambua kilio cha wafanyakazi na katika kuelekea siku ya wafanyakazi wanatarajia kusikia mambo mema na mazuri kutoka kwa serikali iliyoahidi.
“Natumia fursa hii kuwahasa wafanyakazi wenzangu kufanya kazi kwa bidii ili iwe rahisi kwa serikali kuangalia namna bora ya kuboresha maslahi yetu na kikubwa tuchape kazi,”’amesema