Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:29 am

NEWS: NAPE AMTETEA MAMA SAMIA

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Moses Nnauye amesema kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama chao cha Mapinduzi CCM, swala la kukosoa na kujikosoa mwenyewe ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na si dalili ya udhaifu.

Nape ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili 15, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu na taasisi zake kwa mwaka 2021/22.

Amesema Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan ameanza vizuri na kutaka wananchi kumpa ushirikiano, “mzee Mwinyi (Ali Hassan- rais wa awamu ya pili) alituambia kila zama na kitabu chake.”

“Tusigombane bila sababu Tanzania ni yetu sote tumsaidie mama naye aandike kitabu chake tusimshike mkono kumwandikia kitabu tumwache aandike kitabu chake na ndugu zangu legacy (alama) haitetewi inajitetea yenyewe.”

“Hasa ile inayofanywa na mtu kama Magufuli itajitetea na kujisimamia miaka labda kama mtu ana mashaka na legacy yake lakini kama hamna mashaka na legacy yake itasikilizwa, itaongewa sisi watoto wajukuu na vitukuu kwa sababu haya waliyoyafanya watayakuta,” amesema.

kauli hiyo ya Nape imekuja Siku moja mara baada ya kuibuka kundi la wabunge kupinga wale wote wanaokosoa utendaji kazi wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli.

Wabunge hao wamedai kuwa Rais Magufuli alifanya mambo makubwa na ya kihistoria ambayo hayapaswi kubezwa na watu.