Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 2:13 am

NEWS: MUHIMBILI YAKANUSHA KUSAMBAZA PICHA ZA PROFESA JAY

Dar es salaam. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam imekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hukuhu hospitali hiyo kurekodi na kusambaza video na picha za Mwanasiasa na mwanamuziki wa hip hop Joseph Haule Joseph Haule maaruru Profesa J na kusema .

Video hiyo imesambazwa na Mtandao wa Mange Kimambi ikimuonesha Profesa Jay akipatiwa matibabu Muhimbili Hospitali Upanga”

"Uongozi wa Hospitali unatoa taarifa kuwa video hii haijarekodiwa na kusambazwa na Hospitali, tumesikitishwa na tunalaani vikali kitendo hiki cha kumrekodi mgonjwa anayepigania uhai wake ICU na kuisambaza, hiki ni kiwango cha juu cha kukosa utu na maadili"

"Tunafuatilia kwa ukaribu tukio hili ili kubaini chanzo cha video hiyo ili hatua stahiki zichukuliwe, Wananchi endeleeni kuwa na imani na Hospitali ta Muhimbili" imeeleza taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Muhimbili.