- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Mtu aliyepanga kumuuwa Trump afungwa Jela
Nevada Marekani: kijana mmoja raia wa Uingereza amehukumiwa kifungo cha mwaka 1 jela kufuatia jaribio lake la kutaka kumpiga bunduku Donald Trump.
Michael Sandfgord mwenye umri wa miaka 20 alikiri makosa hayo ya kumiliki bunduki na kuvuruga mkutano huo ulikuwa wa kampeni za bwana Trump.
Analaumiwa kwa kujaribu kunyakua bunduki kutoka kwa polisis wakati wa mkutano wa hadhara huko Las Vegas ili kumfyatulia risasi mgombea urais.
Mahakama ilisema kuwa huenda akaachiliwa baada ya miezi minne ambapo atasafirishwa hadi nchini Uingereza
Baada ya Sandford kukamatwa aliwaambia maafisa kuwa alikuwa na mpango wa kumpiga risasi Donald Trump.
Hata hivyo hakufanikiwa kunyakua bunduki kutoka kwa afisa wa polisi.
Mamake alisema kuwa alikuwa amepoteza mawasiliano na mwanawe, ambaye aliondoka nyumbani kutembea kote marekani mwaka 2015Kulingana na nyaraka za mahakama Sandfords ambaye hakuwa na makao na ambaye alikuwa akiishi Marakani kinyume na sheria baada ya muda wa visa yake kuisha, aliiwaambia majasusi kuwa aliendesha gari kutoka California hadi Nevada kwa aengo la kumpiga risasi Trump.
Anaripotiwa kumuambi afisa wa polisi kuwa alitarajia kuuawa kwenye shambulizi hilo na kwamba alikuwa na tikiti za kuhudhuria mkutano mwingine wa Trump baadaye ikiwa angapata furss ya pili.
Majaji walitaja kitendo hicho kuwa cha kustaajabishaBbc/swahili