- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTATURU, “Watanzania tembeeni kifua mbele,Rais Samia yupo,”.
DODOMA: Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amesema kazi nzuri iliyofanywa na Hayati Dkt John Magufuli inaendelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Ilani bora ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akichangia mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu April 14 bungnei jijini Dodoma amesema Dkt Magufuli alifanya mambo mengi ambayo kwa sasa yanaendelezwa na Rais Samia.
Amesema maono ya viongozi wa nchi yanasimamiwa na Ilani bora ya CCM ambayo imepanga mipango na inatafsiriwa katika dira ya maendeleo na mpango wa maendeleo wa miaka mitano mitano.
“Katika maendeleo yaliyofanyika huwezi kuondoa viongozi walioshiriki kwa muda wao katika kuhakikisha wanaisadia nchi hii,Mwenyezi Mungu amemtanguliza mbele ya haki Dkt Magufuli lakini hatutamsahahu kwa kazi kubwa aliyoifanya na legacy yake kamwe haitafutika katika nchi hii,”amesema.
Amesema na ndio maana kama bunge waliazimia kwa pamoja kupongeza na kutambua juhudi zake ili kuweza kuzalisha akina Magufuli wengi zaidi.
“Dkt Magufuli alikuwa jasiri katika kupambana na vita ya ujangili wa tembo, na kila mtu anajua kuwa miaka ya nyuma kulikuwepo na ujangili mkubwa wa tembo hivyo kusababisha kupungua lakini sasa suala hilo kwa kiasi kikubwa limedhibitiwa na kupelekea kuwepo kwa ongezeko,”ameongeza.
Ametolea mfano mwaka mwaka 2014 kulikuwa na tembo karibia 100,009,lakini wamepungua na kufikia 45,000 lakini kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Wizara ya Maliasili leo wamefikia tembo 60,000.
“Hii ina maana kuwa tumeweza kusimamia vizuri rasilimali zilizoachwa nchini,sasa twende kifua mbele, kazi iliyofanyika ni nzuri tusibabaishwe na kelele za pembeni,viongozi wetu wamejipanga vizuri kuhakikisha Tanzania inasonga mbele,”alisema.