Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 2:28 pm

NEWS; MTATURU AWASEMEA WAZEE MATIBABU BURE.

DODOMA; Serikali imeahidi kukaa na kuangalia namna ya kuboresha eneo la utambuzi wa wazee ili kurahisiha upatikanaji wa matibabu.

Ahadi hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dokta Godwin Mollel wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu.

Katika swali lake mbunge huyo ametakak ujua hatua ya ziada inayochukuliwa na serikali katika kuhakikisha wazee wote wanasajiliwa kwa muda uliopangwa ili wapate matibabu.

“Kwa sababu kwenye jibu lake wamesema wanaruhusu kuhakiki wazee na mfumo huo haujawa rasmi umewaachia halmashauri kwa sasa,na hiyo ndio inakwamisha wazee wengi kutopata huduma hiyo kwa kigezo cha kutosajiliwa,Je nini hatua ya ziada ya serikali kuhakikisha wazee wote wanasajiliwa katika muda uliopangwa ili wapate matibabu,?alihoji.

Akijibu swali hilo Dokta Mollel amesema ili kurekebisha hilo watakaa kuona namna bora ya kuboresha eneo hilo la utambuzi.

“Nachukua hoja ya mbunge kwa sababu kuna tatizo kwenye utambuzi wa wazee hivyo tutaenda kukaa kuona tunaboresha eneo hili ili kujua nani mzee na nani sio mzee,lakini suala hapa ni kupata tiba,sasa tunapokwenda kwenye muswada wa bima ya afya kwa wote hilo litakuwa limeingia kwenye utaratibu mzima hivyo halitakuwa na shida,”alisema.