- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS; MTATURU ASISITIZA MAMBO MATATU KWENYE KILIMO.
DODOMA; Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameiomba serikali kuweka msisitizo katika mambo matatu ili kumsaidia mkulima kupata tija katika kilimo anachofanya na hivyo kuiwezesha sekta ya kilimo kuwa na mchango zaidi katika pato la Taifa.
Msisitizo huo ni kwenye utafiti wa mbegu,kilimo cha umwagiliaji na kupunguzwa kwa masharti katika benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB).
Akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara ya Kilimo ya Mwaka 2021/2022,Mei 24 bungeni,Mtaturu amesema ni ukweli usiopingika kwamba Kilimo ndio kimebeba uchumi wa nchi kutokana na asilimia 80 ya watanzania kujishughulisha na shughuli za kilimo.
“Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali,tusipokuwa na mbegu bora hatuwezi kuwa na kilimo chenye tija,wananchi watapoteza muda wao nguvu zao nyingi na hatutaweza kwenda mbele bila ya kuwa na mbegu bora,”alisema.
“Nitolee mfano kwenye zao la alizeti,leo hii tunalia wote kwamba tunatatizo kubwa la mafuta ya kula,serikali inatumia fedha nyingi za kigeni kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi ilhali tuna ardhi ya kutosha ,tuna mazao mengi yanayoweza kutoa mbegu za mafuta,niiombe serikali tuongeze nguvu kwenye eneo hili ,
Jambo la pili aliloliwekea msisitizo ni kuhusiana na kilimo cha umwagiliaji na kuiomba serikali kupitia maafisa biashara,maafisa kilimo na maafisa mipango kwenye halmashauri kusimamia vizuri suala la masoko ili kumfanya mkulima afaidike na kilimo chake.
“Kilimo cha umwagiliaji kipewe nafasi,hekta zinazotengwa hazitoshi,lakini pia eneo hili tuongeze wataalam wa kutosha kwenye halmashauri zetu,leo hii unaweza kusema unaweka skimu ya umwagiliaji unawakabidhi wakulima ambao wao wenyewe hawana uwezo wa kuendesha mradi ule ,tunapoteza fedha,
“Tumesikia kuna tume ya umwagiliaji inaboreshwa niiombe sana nguvu ziongezeke tuwaweke wataalam mule wapangwe kwenye halmashauri zetu wasimamie ,kilimo hiki tukifanya vizuri tutatumia eneo dogo na tutapata uzalishaji mkubwa,leo nchi inapata mvua kubwa katika baadhi ya maeneo mpaka inaharibu miundombinu,niiombe serikali iweke nguvu kwenye kuvuna maji ya mvua,ijenge mabwawa yakutosha,”ameongeza.
Mtaturu ametolea mfano kwenye zao la alizeti katika mkoa wa Singida ambapo baadhi ya maeneo wakulima wanakopwa wakiwa bado shambani hajavuna na hivyo kupelekea kuuza kwa bei ya kutupa na hivyo kumfanya kutorudi shambani.
Amezungumzia kuhusu Benki ya TADB ambayo imepewa fedha na serikali ili kuwakopesha wakulima lakini masharti yake yaliyopo sio rafiki kwa wakulima waliopo vijijini.
“Mie ninayo Amcos moja pale Misughaa Ikungi,wamekopeshwa Mil 85 tu, leo tunavyoongea kwa sababu msimu uliopita haukuwa na mvua ya kutosha wamepelekwa TAKUKURU ,wamepelekwa Mahakamani,yaani ni kama vile hapakuwa na mkataba ,
“Kwa hali hii usitegemee wakulima hawa mwakani wataenda kwenye benki hiyo,nitakukabidhi waziri ili ufuatilie ,haiwezekani watu waliokuwa na mkataba wa makubaliano ya mkopo na wamekubaliana kwamba watu wa Bima wapolakini mwisho wa siku wasipovuna vizuri wanapelekwa Takukuru,wanapelekwa mahakamani haiwezekani ,unamfanya huyu mkulima aogope kwenda kukopa tena,”aliongeza.
Ameiomba serikali pamoja na juhudi zinazofanyika za kuongeza fedha lakini huduma inayotolewa sio nzuri na haimsaidii mkulima bali inaenda kumnyonya na kumtoa kwenye mawazo mazuri aliyokuwa nayo.
“Niiombe serikali tuwawekee mazingira mazuri ya kuwawezesha kuwa na uwezo wa kulima eneo kubwa,tuwape pembejeo za kutosha na vifaa ikiwemo matrekta ili wabadilishe kilimo chao kutoka kwenye kilimo cha kawaida,”alisema Mtaturu.