- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS; MTATURU ASHIRIKI UJENZI WA OFISI YA CCM WILAYA YA IKUNGI.
SINGIDA; Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki uzinduzi wa ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ),wilaya ya Ikungi inayotarajiwa kugharimu jumla ya Sh Milioni152.
Akizungumza katika uzinduzi huo Juni 12,Mtaturu amesema ameshiriki ujenzi huo Ili kuonyesha dhamira ya dhati aliyonayo katika kuhakikisha Ofisi hiyo inajengwa na kukamilika kwa muda uliopangiwa.
"Ili kuhakikisha dhamira hii inafanyika kwa vitendo nimechangia bati 100 na saruji mifuko 100 vyenye thamani ya Sh Milioni 5.9,na hii sio mwisho nitaendelea kuunga mkono ujenzi huu kwa kadri Mungu atakavyonijalia,
"Mwenyekiti wetu wa CCM wilaya,leo tunapata heshima kupitia wewe,tunajivuni ulituongoza kwa busara na hekima ,sisi CCM ni kiongozi ,tulijua ukweli kuhusu eneo hili lakini kwa kuwa ni Chama kinachozingatia utawala Bora tulitulia,CCM inafuata kanuni,Sheria na taratibu,sasa niahidi kuwa nitahamasisha wadau wote ,uzuri wa jambo hili lazima tufanye wote,CCM ni Chama Cha wananchi kila mmoja anapaswa kushiriki,"aliongeza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ambaye ndie alikuwa mgeni Mika Likapakapa amewapongeza wanachama na viongozi kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki ujenzi huo.
"Niwaombe wanachama na viongozi kuendelea kutoa michango mbalimbali ili kufikia lengo la ofisi kukamilika ifikapo October 2021,niwashukuru wabunge na wadau mlioanza kuchangia ujenzi wa ofisi hii,"alisema.
Nae Katibu wa CCM wilaya hiyo ya Langael Akyoo amesema uongozi wa CCM wilaya umeazimia kuanza ujenzi huo mara moja.
"Wilaya ya Ikungi ilianzishwa mwaka 2012 na dhamira ya kujenga Ofisi ilikuwepo ila ilikwamishwa na mgogoro wa kiwanja hicho ambacho na hukumu ya mahakama iliyotolewa mwezi Mei, 2020,"alisema .
Amesema ramani ya Ofisi hiyo inahusisha Ofisi za Jumuiya zote tatu wilaya,ukumbi wa mikutano na vyumba vya biashara.