Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:29 pm

NEWS; MTATURU ARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAJI KATA YA DUNG'UNYI

SINGIDA; Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amekagua ujenzi wa miradi ya maji katika Kata ya Dung'unyi na kuonyesha kuridhishwa na utekelezaji wake.

Aidha,katika ziara hiyo amechangia takribani ''Milioni sita*katika miradi ya maendeleo''

Akizungumza katika ziara hiyo Mei 29,2021,Mtaturu amesema katika miradi ya Maji Serikali imepeleka kiasi Cha Bilioni 1.6 na kusaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji iliyokuwepo awali.

"Ndugu zangu,Chama Cha Mapinduzi kina dhamira ya dhati ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani Kama Ilani ilivyoahidi,na niwaahidi hapa kuwa tutaongeza vituo vya kuchotea maji,

" Niwaombe pia tuache maneno maneno,mwenye nyumba ni CCM na tupo salama,"aliongeza Mtaturu.

Amempongeza Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Wakala wa Maji na Usafiri wa Mazingira Vijijini (RUWASA), wa wilaya ya Ikungi kwa kusimamia ujenzi wa miradi hiyo.

Akizungumzia kuhusu fedha alizotoa kusaidia miradi ya maendeleo amesema,Shilingi Milioni moja amechangia kwenye ujenzi wa jengo

la mama na mtoto linalojengwa katika Zahanati ya Dung'unyi ili kuunga mkono juhudi za wananchi.

"Niwapongeze wananchi kwa moyo wenu wa kujitolea uliokuwa umefifia miaka ya nyuma,nimetoa kiasi hiki Cha fedha Ili kuunga mkono juhudi zenu,

"Mbali na fedha hii,nimekabidhi pia viti 100 kwenye kanisa Katoliki la Dung'unyi,

Sh 500,000 nimechangia ujenzi wa nyumba ya mchungaji kanisa la KKKT na nimetoa mbao za kupaulia msikiti wa mtaa wa Dung'unyi zenye gharama ya Sh Milioni 1.8,yote nimefanya kutokana na juhudi zenu mlizozionyesha,"alisema.

Mbali na hayo ametoa vifaa na michezo ambavyo ni jezi seti tano na mipira mitano kwa timu za vijiji vitano ili kusaidia kuinua michezo na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuibua vipaji vya vijana.