- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTATURU AIOMBA SERIKALI KULITAFUTIA SULUHU SUALA LA BANDARI YA DAR ES SALAAM.
BUNGENI DODOMA: Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amekuwa miongoni mwa wabunge waliyoiomba serikali kuliangalia suala la Bandari ya Dar es salaam ambayo malori yameshindwa kushusha na kupakia mizigo kwa takribani siku tano hadi sita sasa.
Akiunga mkono hoja iliyotolewa na mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi Mei 11 bungeni,Mtaturu amesema fedha nyingi zimewekezwa kwenye bandari hiyo.
“Tumewekeza fedha nyingi katika kuboresha bandari ya Dar es salaam,kuanzia gati namba moja hadi kumi,,tunashukuru wengine sie ni wajumbe wa kamati ya miundombinu hivyo tumeshuhudia kwa macho uboreshaji uliofanyika, leo hii kukiwa na tatizo kunaathiri sana uchumi wetu,
“Ni vizuri serikali ikatuambia ni juhudi gani zinafanyika kuhakikisha inakwamua hali hii, kijiografia bandari yetu ya Dar es salaam ipo vizuri ila ni vyema tukaboresha usimamizi wake ili kuendelea kukuza uchumi wan chi,ninaiomba serikali ichukue hatua stahiki ili kuokoa uchumi wan chi yetu,”alisisitiza.
Katika hoja yake mbunge Chumi aliliomba bunge kusitisha shughuli zake Ili kujadili suala hilo ambalo linaathiri uchumi wa Nchi.