Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 2:13 am

NEWS: MTATURU AIOMBA SERIKALI KUKAMILISHA SKIMU YA MANG'ONYI,SINGIDA.

DODOMA: Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu, ameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Mang’onyi ili kuongeza tija ya kilimo cha mboga mboga katika kata za Mang’onyi na Makiungu.

Mtaturu ametoa ombi hilo bungeni Februari 3,2021, wakati akiuliza swali lanyongeza.

"Kilimo cha umwagiliaji kinatija na soko la mbogamboga ni kubwa hasa ikizingatiwa Mgodi wa Shanti utaanza kufanya kazi hivi karibuni,je serikali haioni umuhimu kwa sasa kutenga fedha ambazo zilikadiriwa Sh.Milioni 580 ili kukamilisha upande uliokuwa umebakia wa banio?,”amehoji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde, amesema skimu hiyo imeendelezwa kwa kujengewa banio linalopokea maji kutoka bwawa la myanji na takribani hekta 50 kati ya hekta 450 zimeendelezwa kwa kujengewa miundombinu ya umwagiliaji na sehemu ya shamba lililobaki hufikiwa na maji kwa njia ya asili.

Aidha amesema serikali inatambua umuhimu kwenye kilimo cha umwagiliaji na katika bajeti ijayo zitatengwa fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi huo.