- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS; MTATURU AIBANA SERIKALI KUHUSU UMEME JIMBONI.
BUNGENI DODOMA; Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itafikisha umeme katika vijiji 28 ambavyo bado havijapatiwa umeme kati ya vijiji 50 vya jimbo hilo.
"Jimbo la Singida Mashariki lina vijiji 50,vijiji 28 Kati ya hivyo havijapatiwa umeme,je ni lini vijiji hivyo vitapatiwa umeme,? Alihoji.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato, amesema serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kupeleka umeme vijijini na kuufikisha katika vijiji vyote vya Tanzania Bara ifikapo mwezi Desemba, 2022.
“Vijiji 12 vinapatiwa umeme kupitia Mradi wa Ujazilizi ulioanza kutekelezwa katika Mkoa wa Singida mwezi Novemba, 2020 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2021,
"Vijiji 16 vilivyobakia vitapatiwa umeme kupitia utekelezaji wa mradi wa REA wa kusambaza umeme vijijini awamu ya Tatu mzunguko wa Pili ulioanza kutekelezwa mwezi Machi, 2021 na utakakamilika mwezi Desemba 2022,".
Byabato amesema gharama ya mradi ni Sh.Bilioni 8.47.