- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS; MTATURU AIBANA SERIKALI KUHUSU AFYA SINGIDA MASHARIKI.
DODOMA; Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itajenga vituo vya afya Issuna,Ikungi,Makiungu,Ntuntu na Misughaa ili kurahisisha huduma za dharura Wilayani Ikungi kwa kuwa Wilaya hiyo inapitiwa na barabara ya Dodoma -Mwanza na kumekuwa na ajali za mara kwa mara.
Aidha, ametaka kujua sababu ya serikali kutopeleka gari la wagonjwa kwa ajili ya kuwahamisha majeruhi na wagonjwa katika Hospitali za Rufaa.
Akijibu maswali hayo Juni 23 bungeni Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Dokta Festo Dugange amesema serikali inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi iliyoanza kujengwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo hadi mwezi Mei 2021 ilikuwa imepatiwa Shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi.
Aidha, amesema Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga Shilingi milioni 800 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo ikikamilika itasaidia kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali zitakazotokea eneo la Ikungi katika Barabara ya Dodoma hadi Mwanza.
Dokta Dugange amesema kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Mei 2021 Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya Ihanja na Sepuka ambapo ujenzi wa Vituo hivyo umekamilika na vituo vinatoa huduma ikiwemo huduma za dharura za upasuaji.
“Kwa hivi sasa serikali inapitia sera ya zahanati katika kila Kijiji na kituo cha afya katika kila kata na itafanyiwa maboresho yenye tija zaidi ili ujenzi uwe wa kimkakati badala ya kila kijiji au kila kata,”alisema.
Akizungumzia kuhusu gari la kubebea wagonjwa amesema Halmashauri ya Wilaya Ikungi ina magari matatu ya kubebea wagonjwa ambayo yapo katika Vituo vya Afya Ikungi, Sepuka na Ihanja ambayo yote yanaendelea kutoa huduma za rufaa za dharura ndani na nje ya wilaya ya Ikungi.
Katika swali la nyongeza Mtaturu ametaka kujua mpango wa serikali wa kujenga vituo vya afya ikiwemo Kata ya Makiungu,Ntuntu ambayo ni ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyowahi kuitoa wakati wa kampeni.
“Jimbo la Singida Mashariki lina kata 13 na tuna kituo cha afya kimoja ambacho pia hakina huduma nzuri,Je serikali ina mpango gani wa kujenga vituo vya afya vingine katika kutekeleza mpango wake wa kujenga kituo Cha afya kimoja katika kila kata,”alihoji.
Pia Katika swali lake la pili amehoji,“Ni kweli mmeleta fedha ya kujenga hospitali ya wilaya alkini fedha hizo zilirudishwa baada yam waka wa fedha kupita,na hivi sasa ni Zaidi ya miezi sita fedha hizo hazipo na ujenzi umesimama,je ni lini serikali italeta fedha hizo ikiwemo kuleta vifaa kwa ajili ya vifaa tiba ili iweze kutoa huduma,”alihoji.
Akijibu maswali hayo Dokta Dugange amesema sera ya maendeleoo ya afya ya msingi inaenda kuboresha ili kuwa na tija,uhalisia na ufanisi mkubwa Zaidi.
“Tuna vijiji karibu 12,000,mitaa 4,000,kata 3956 hivyo tunataka kwenda kimkakati zaidi kujenga vituo vya afya katika maeneo ya kimkakati vitakavyokuwa na kila kitu na hii itatoa tija zaidi badala ya kujenga kila kata na kila kijiji,”alisema.
Amemhakikishia mbunge kuwa vituo hivyo vya afya ambavyo ni ahadi ya Rais Samia aliyoitoa vitajengwa ikiwemo na vituo vyote vitakavyofanyiwa tathimini nakuona tija ya kujengwa ipo vitajengwa ambapo mpango utaendelea kutekelezwa kwa utaratibu huo.
“Fedha za ujenzi wa hospitali zilizorejeshwa kwa kipindi hicho zilirejeshwa kwa mujibu wa sheria ya bajeti ya mwaka 2015 lakini serikali imeshafanyia maboresho na waheshimiwa wabunge tumesikia katika mwaka wa fedha ujao fedha zinazopelekwa katika miradi ya maendeleo hazitarejeshwa baada ya tarehe 30 Juni,nimhakikishie mbunge kuwa fedha hizo tutafanya utaratibu wa kuzirejesha ili kuendelea na ujenzi wa hospitali kama ulivyopangwa,”alisisitiza .