Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 1:23 am

NEWS: MTATURU AIBANA SERIKALI BUNGENI.

DODOMA: Serikali imewahakikishia wakazi wa Mji wa Ikungi kuwa ahadi ya ujenzi wa kilomita tano za barabara kwa kiwango cha lami itatekelezwa chini ya serikali ya awamu ya sita.


Ahadi hiyo imetolewa April 21,2021 bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)David Silinde kufuatia swali la mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu.

Katika swali lake mbunge huyo ameihoji serikali ni lini itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo ili nao wafaidi matunda ya Uhuru.

“Kwa sababu Mji wa Ikungi ni wilaya mpya,na kwa sababu makao makuu ya wilaya tunategemea yawe na lami ,na Mhe Waziri Mkuu mwaka 2019 alituhakikishia kujengwa kwa barabara hiyo na leo ni 2021,ni lini sasa fedha zitatengwa,?”alihoji.

Akijibu swali hilo Silinde amesema Serikali itaendelea kufanya usanifu na kujenga barabara kwakiwango cha lami kwenye maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Ikungi kulingana na upatikanaji wa fedha.

“Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali kupita Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imepanga kufanya usanifu na tathmini ya gharama za ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami katika Mji wa Ikungi,utambuzi wa barabara hizi utakuwa shirikishi ili kutoa kipaumbele kwenye barabara zenye umuhimu mkubwa,”.

Amesema hadi Machi Machi 2021, TARURA imetoa Shilingi milioni 598.22 kati ya Shilingi milioni 890.89 zilizotengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 97.92 katika ya Wilaya ya Ikungi.

Aidha, Shilingi bilioni 1.4 zitatengwa kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mihyuge Wilayani Ikungi.

“Mara baada ya usanifu na tathimini ya kina itakayofanyika katika mwaka huu fedha kukamilika tutaanza kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa lami,”alisisitiza.