Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:26 am

NEWS: MTANZANIA ASHINDA TUZO YA HESHIMA NOBEL

Mtanzania Abdulrazak Gurnah Mtunzi wa vitabu mbalimbali vya fasihi amefanikiwa kushinda Tuzo ya amani ya Fasihi ya Nobel kwa mwaka 2021.

Tuzo hiyo imetangazwa mjini Stockholm Sweden na Katibu wa Kudumu wa Swedish Academy Mats Malm.

Gurnah alizaliwa Zanzibar mwaka 1948, ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Kent, Uingereza,

Anakuwa Mwandishi wa kwanza wa Kitanzania na mwandishi wa pili mzaliwa wa bara la Afrika kushinda tuzo hiyo.

Tuzo hiyo Nobel inaambatana na zawadi ya medali ya dhahabu na fedha taslimu ya Dola $1.14m ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 2.62 za kitanzania.

Gurnah anafahamika kwa riwaya yake iitwayo Paradise.

NobelPeacePrize