Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:26 pm

NEWS: MTANDAO WAKWAMISHA KESI YA MBOWE KISUTU

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam imeshindwa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa chama kikuu cha Upinzania nchini Tanzania Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, mara baada ya mtandano wa internet kwa njia ya video conference kuwa hafifu.

Mbowe anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kula njama za kutenda kosa na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za Ugaidi, huku wenzake watatu wakikabiliwa na mashtaka saba.

Baada ya hitilafu hiyo ya Kiufundi kutokea Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, ambaye anasikiliza shauri hilo, Thomas Simba, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 6, 2021.

Kabla ya kuahirisha kwa kesi hiyo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hila akisaidiana na Christopher Msigwa na Grace Mwanga, ameieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kutajwa.

Kwa upande wa washtakiwa wao, wanatetewa na jopo la mawakili watano ambao ni Peter Kibatala, John Mallya, Jonathan Mdeme, Fedreck Kiwelo na Sist Aloyce.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.