- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSIGWA AWATAKA VIJANA KUFANYAKAZI KWA WELEDI KWA MASLAHI YA TAIFA
DODOMA: Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo , Gerson Msigwa amewataka Vijana nchini kufanyakazi kwa matarajio, mategemeo ya Rais Samia Suluhu Hassan nakwamasilahi ya Taifa ili kuepuka kuwa Vijana wa hovyo.
Msigwa ameyasema hayo leo Ijumaa Desemba 13,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kukabidhiwa Idara ya Habari kutoka iliyokuwa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Amesema Rais Samia amekuwa akiwaamini vijana na kuwapa nafasi namajukumu makubwa changamoto ni kufanyakazi kwa Matarajio ya Mhe. Rais na mategemeo yake.
Pamoja na hayo amewataka waandishi wa Habari nchini kutumia kalamu zao kuandika habari zitakazosaidia kuilinda nchi na kukataa kutumia kalamu zao kuandika habari za kuvuruga tunu za taifa ikiwemo amani na utulivu.
Aidha, amesema "Waandishi wa habari ni nguzo muhimu katika kulinda utulivu na maendeleo ya taifa. Tuendelee kuisaidia serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za pamoja,".
Pamoja na hayo ametoa shukrani kwa Rais Samia kwa kuwaamini vijana na kuwapa nafasi za uongozi, akibainisha kuwa uteuzi wa kwake na wa Makoba ni mfano wa kuigwa.
"Kwa niaba ya vijana wenzangu, tunamshukuru Rais kwa kutuamini. Kazi yetu sasa ni kuhakikisha tunafanya kazi kwa bidii ili tusije kuwa 'vijana wa hovyo,'" amesema Msigwa.
Kwa upande wake aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali,Thobias Makoba amewashukuru Waandishi wa Habari kwa uzalendo wao wanaoendelea kuuonesha kwani bila uzalendo, kalamu ya mwandishi inaweza ikabomoa jamii huku akitolea mfano waandishi walivyoshiriki kutoa taarifa zilizo sahihi kwa jamii yalipotokea maafa ya kudondoka kwa ghorofa Kariakoo.