- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSIGWA ALISHAURI BUNGE KUTUNGA SHERIA ZISIZO NA UKANDAMIZAJI
MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa(CHADEMA), amelishauri Bunge kutunga sheria ambazo hazitakuwa mzigo kwa Watanzania.
Mchungaji Msigwa ametoa ushauri huo leo Juni 10,2020 Bungeni Mjini Dodoma wakati anachangania Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali ambao umewasilisha Bungeni.
"Moja ya jukumu la msingi la Bunge ni pamoja na kusimamia utungwaji wa sheria,hivyo wabunge wanao wajibu wa kusimamia utungwaji wa sheria ambazo hazitakuwa za ukandamizaji,"amesema Mchugaji Msigwa.
Amongeza hivyo ni makosa kuwa na sheria au mabadiliko ya sheria katika nchi bila wananchi kujua."Hivyo ni vema tuwe na sheria rafiki kwa wananchi."
Amesema sheria hazina macho na wala haziangalii aliyeko sasa peke yake, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisheria kabla ya kutungwa inakuwa imekamilika na iko sawa sawa.
"Kuna kila sababu ya kuangalia kwa undani zaidi sheria ambazo zinatungwa na Bunge ili kuwa na tija kwa Watanzania wote kwani lengo la kuwa na sheria sio kutesa wananchi,"amesema Mchungaji Msigwa