Home | Terms & Conditions | Help

April 6, 2025, 6:55 am

NEWS: MSANII WAKAZI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KUPITIA ACT

Msanii wa HipHop nchini Tanzania Wakazi ametia nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Segerea kupitia chama cha ACT Wazalendo kwenye uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Wakazi ameeleza nia hiyo leo Juni 20, 2020 kwenye mkutano wa chama hicho unaofanyika jijini Dar es salaam wakati wa Kutambulishwa na kuwapokea wabunge 21 kutoka chama cha CUF.

Wakazi amesema amekuwa mwanaharakati wa muda mrefu wa masuala ya haki na usawa hivyo ameona ni wakati sasa wa kuwa kiongozi.

”Kwasababu nimepata heshima ya kuitwa hapa mbele ya mkutano naomba nitumie nafasi hii kutangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge katika Jimbo langu la Segerea”, amesema.

Wiki hii msanii Wakazi alikabidhiwa kadi ya chama hicho na Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe.