Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:49 am

NEWS: MSANII MENINA AIBURUZA DSTV MAHAKAMANI

Msanii wa Bongofleva, Menina Abdulkarimu Atiki ameipeleka mahakamani kampuni ya ving’amuzi ya DSTv, MultiChoice South Africa na mbia wake nchini Tanzania, MultiChoice Tanzania kupitia chaneli yao ya Magic Bongo akiidai fidia ya Tsh1.12 bilioni kwa madai ya kumkashifu(defamation).

Menina ambaye pia anafanya kazi ya ushereheshaji na balozi wa bidhaa mbalimbali nchini ameishtaki kampuni hiyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, akiwakilishwa na wakili, msomi John Mallya.

Menina anaishtaki DSTV mara baada ya Chaneli ya Magic Bongo kupitia kipindi cha ICU chumba cha umbea kurusha maudhui ya kumdhalilisha na kumkashifu msanii huyo siku chache baada ya kufiwa na mumewe Mussa.

Katika kipindi hicho kinaWatangazaji kama Maimartha Jesse, Juma Lokole na Kwisa Thompsn maarufu Kamanda Mzee Mkavu.

Katika hati ya madai ya kesi hiyo namba 133 ya mwaka 2021, msanii huyo anadai kuwa wadaiwa hao walimkashifu kutokana na maudhui waliyoyarusha Julai 23, 2021 katika kipindi hicho kuhusu kifo cha mumewe.

Menina anaeleza kuwa mumewe alifariki dunia Julai 19, 2021, familia yake na ya mumewe zilikubaliana maziko yafanyike Mtoni kwa Aziz Ali, nyumbani kwa shangazi wa marehemu, Mariam Kihiyo.

Amedai kuwa wakati mazishi yakiendelea, Maimartha, Lokole na Kwisa waliwahoji majirani wa shangazi wa marehemu kwa nia ovu walipenyeza maneno yaliyowachochea kutoa maneno kuonyesha kuwa hakuwa na upendo kwa mumewe, huruma wala maadili na alikuwa akimnyanyasa mumewe.

Aidha watangazaji wa kipindi hicho walikwenda kinyume cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 vigungu vya 35 na 39

"Hairuhusiwi kuchapisha ama kutangaza habari zenye kukashifu isipokuwa tu iwapo habari hizo ni za kweli na zinabeba maslahi ya umma".

Sheria inaeleza mazingira ambayo kuchapisha habari au taarifa za kashfa hakutochukuliwa kama ni kuvunja sheria, na ambayo mwanahabari husika hatoadhibiwa – hasa pale ambapo habari au taarifa husika inachapishwa na mamlaka za Serikali. Kuchapisha au kutangaza habari zinazohusu kashfa unaruhusiwa katika mazingira mbalimbali, hasa iwapo kutangaza au kuchapisha habari hizo kunafanywa kwa nia njema.