Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 4:02 pm

NEWS: MSAJILI AIKALIA KOONI CHADEMA, AIONYA VIKALI

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Mstaafu Francis Mutungi, amekionya vikali Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutokana na alichodai kuwa ni uvunjifu wa Sheria kwa kuongeza Beti ya tatu kwenye wimbo wa Taifa wa Tanzania.

Chadema kimedaiwa kuongeza ubeti huo jana Agosti 3, 2020 wakati chama hicho kikiendelea na vikao vyake vya ndani vya baraza kuu la chama hicho la kumtafuta mgombea nafasi ya uras wa Jamhuri na Zanzibar.

Jaji Mutungi ametoa onyo hilo leo Agosti 4, 2020, huku akisema kuwa hakutegemea kwa chama kikongwe kama chadema kufanya kitendo hicho.

Jaji Mutungi ameongeza kuwa kwa mujibu wa katiba ni kosa, huku akivikumbusha vyama vya siasa vyote vinavyoendesha michakato katika vyama vyao kukumbuka kwamba sheria hazijakwenda likizo.