- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MPANGO ATAKA USAWA KATIKA NYANJA ZOTE BARANI AFRICA
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema ili kufikia ajenda ya Afrika Tuitakayo, Bara la Afrika linahitaji usawa katika uongozi, uwakilishi sawa katika masuala ya siasa pamoja na mazingira ya usawa katika masuala ya kijamii na kiuchumi.
Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha awali cha nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika cha jukwaa la kujadili masuala ya usawa wa kijinsia, kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao.
Amesema kwa upande wa Tanzania, Serikali inatambua kuwa usawa wa kijinsia pamoja na uwezeshaji Wanawake kiuchumi ni nguzo muhimu katika kufikia maendeleo endelevu kwa jamii yeyote ile, ndio maana imekua ikiingia katika mikataba ya kitaifa, kikanda na kimataifa inayohusu kuimarisha usawa wa kijinsia, kuwawezesha Wanawake kiuchumi pamoja na kuimarisha uwezo wa Wanawake katika uongozi na nafasi za maamuzi katika sekta zote za maendeleo.