Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 7:46 am

NEWS: MORRISON ASHINDA KESI DHIDI YA YANGA.

Mahakama ya usuluhishi wa Kimichezo Duniani (CAS) leo imetoa hukumu ya kesi yenye tatizo la mkataba iliyokuwa ina mkabili Mchezaji wa Simba SC raia wa Ghana Bernard Morrison dhidi ya Club yake ya zamani ya Yanga SC.

Kesi hiyo ilikuwa inahusiana na madai ya Yanga kuwa Morrison anapaswa kuilipa yanga fidia ya USD 200,000 (Tsh milioni 460.2) kwa madai ya kuvunja mkataba na club hiyo bila kufuata utaratibu na kujiunga na Simba SC.

CAS wameweka wazi Morrison alijunga Simba SC kama Mchezaji huru na mkataba wake na Yanga ulikuwa umeisha