- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MMILIKI WA WHATSAPP NA FACEBOOK AINGIA HASARA YA DOLA 7 BILIONI
Huduma katika mitandao ya kijamii kama Facebook, WhatsApp na Instagram zimerudishwa baada ya kukatika kwa karibu masaa sita, jana Facebook imesema.
Kampuni hiyo inasema sababu kubwa nikwamba ilikuwa mabadiliko yaliyofeli ya mfumo wa kimtandao.
Huduma zote tatu zinamilikiwa na Facebook na hazikuweza kupatikana kwenye wavuti au kwenye programu za simu za mkononi.
Baada ya tatizo hilo la kiufundi mmiliki na Mwanzilishi wa mitandao hiyo mark zuckerberg alipoteza kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 7 sawa na takribani Trilioni 16 za kitanzania.
Downdetector, ambayo inafuatilia kukatika kwa huduma za mitandao ya kijamii ilisema ni hitilafu kubwa zaidi kuwahi kutokea, na ripoti milioni 10,6 za matatizo kutoka kwa wateja kote ulimwenguni.
Katika taarifa Jumanne, Facebook ilisema kuwa mabadiliko mabaya ya usanidi yaliathiri zana na mifumo ya ndani ya kampuni ambayo ilikuwa vigumu kujaribu kusuluhisha shida.
Iliongeza kuwa hakuna "ushahidi kwamba data ya watumiaji imeathiriwa kutokana na wakati huu kukatika kwa huduma ".
Siku ya Jumatatu, Facebook ilituma ujumbe wa kuwaomba msamaha kwa wale walioathiriwa na kukatika kwa huduma zake .
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Watu wengine pia waliripoti shida kutumia huduma nyingine zinazotegemea Facebook kama Oculus, na programu ambazo zinahitaji kuingia kwa Facebook ziliathiriwa, pamoja na Pokémon Go.
Kukatika kwa kiwango hiki kwa muda mrefu ni nadra. Usumbufu mnamo 2019 uliacha Facebook na programu zake zingine kutoweza kufikiwa kote ulimwenguni kwa zaidi ya masaa 14.
Kampuni zingine kadhaa za teknolojia, pamoja na Reddit na Twitter, zilichekelea facebook kwa shida hizo - ikisababisha majibu kutoka kwa programu zilizoathiriwa.