Home | Terms & Conditions | Help

January 22, 2025, 1:45 pm

NEWS: Mkutano wa tano wa bunge la Jamuhuri kuanza leo mjini DODOM

Dodoma: Mkutano wa tano wa Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA unaanza leo Mjini DODOMA. huku kukiwa na majukumu matatu makubwa ya kujadili, likiwamo swala la muswada wa sheria wa mwaka 2016

Mkutano wa Tano wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA unaanza leo Mjini DODOMA ambapo pamoja na mambo mengine utajadili miswada miwili ya sheria ukiwemo ule wa huduma za habari wa mwaka 2016.

Spika wa Bunge JOB NDUGAI amesema bunge pia litajadili mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Jumuiya ya Ulaya na nchi za AFRIKA Mashariki – EPA.Kwa mujibu wa Spika NDUGAI, wakati wa majadiliano hayo Wabunge watapata fursa ya kutoa ushauri kwa serikali kuhusu Mkataba huo wa makubaliano.

Ameongeza kuwa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nayo itawasilishwa Bungeni wakati wa mkutano huo wa Tano wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA.