- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKUFUNZI MBARONI KWA KUOMBA RUSHWA YA NGONO
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU ) Mkoa wa Kagera, imesema inamshikilia Mwanaume mmoja jina Ruta Kyaragaine (59) ambaye ni mkufunzi wa Chuo cha Kilimo Maruku, Bukoba, kwa tuhuma za kumuomba rushwa ya ngono mwanachuo wa kike ambaye jina lake limehifadhiwa, kwa lengo la kumsaidie kufaulu mitihani yake ya Mwisho.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera John Joseph amesema leo kuwa mtuhumiwa huyo Ruta Kyaragaine (59) amekuwa akimtisha mwanachuo huyo kuwa asipomkubalia kumpa anachotaka atasababisha ashindwe kufaulu mitihani siku zote.
"Kufuatia kupokelewa kwa taarifa hiyo, tulianza kufanya uchunguzi na tarehe 03/04/2021 tulimkamata mkufunzi huyo akiwa katika nyumba ya kulala wageni iliyoko katika Manispaa ya Bukoba jina linahifadhiwa, akiwa na mwanachuo huyo" amesema Joseph.
Mkuu huyo wa Takukuru amesema wanaendelea na uchunguzi na uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.
John amewaasa wananchi wengine kuacha matendo ya Rushwa kwa linaathiri taifa kwa ujumla wake.