Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 2:41 am

NEWS: MFANYABIASHARA MBARONI KWA KUKUTWA NA DOLA FAKE

Tabora. Mfanyabiashara mmoja ambaye ni Mkazi wa Nzega, Edson Mathayo (33) anashikiliwa na Jeshi Polisi Mkoani Tabora baada ya kukutwa na Dola bandia za Kimarekani 4,600 zenye thamani ya sawa na TSh10.6 milioni kwa fedha za Kitanzania.

Akizungumza na waadishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara amekeamatwa leo Alhamisi Desemba 30, 2021 wakati akienda kubadilisha Dola hizo bandia katika tawi la benki lililopo Manispaa ya Tabora.

"Mfanyabiashara huyo alienda kubadilisha Dola hizo na ndipo alipokamatwa kabla ya kutimiza azma yake " Amesema Kamanda Abwao

Amesema kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi katika kituo kikuu cha Tabora.

Wakati huo huo, mkazi wa Manispaa ya Tabora, Rahim Mohamed (26) amekamatwa na mali mbalimbali zinazodaiwa kuwa za wizi.

Kamanda Abwao amesema mkazi huyo amekamatwa eneo la Kwihara akiwa na sabufa mbili na spika zake nne, pasi moja na runinga moja.