Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 2:05 am

NEWS: MFALME ZUMARIDI AFIKISHWA KORTINI NA WAUMINI WAKE

Mwanza. Mchungaji Diana Bundala maarufu kama 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 92 wamefikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayokabili.

Watuhumiwa wote 92 wanakaabiliwa na kesi tatu ikiwamo ya usafirishaji haramu wa binadamu.

Makosa mengine ni pamoja na shambulio la kudhuru mwili na kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao.

Msafara wa kuwaleta watuhumiwa hao Umewasili katika mahakama hiyo saa 9:00 mchana ukiwa umeongozana na Magari matatu ya polisi aina ya defand kisha watuhumiwa hao kuamuriwa kuingia ndani ya mahakama hiyo.

Akishuka katika gari ya polisi iliyokuwa imembeba, Zumaridi amesikika akisema "Mimi ndiyo Mfalme Zumaridi" huku akionyesha ishara ya kuomba.

Akiwasomea mashitaka hayo mahakamani hap oleo Machi 3, Mwendesha mashtaka wa Serikali amesema katika kesi namba 10/2022 inayomkabili Mfalme Zumaridi peke yake, akidaiwa kusafirisha binadamu wakiwemo watoto wenye umri chini ya miaka 18 kinyume cha kifungu namba 4(1) (A) na 6(2) (A) cha sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu namba 6 ya mwaka 2008.

Katika kesi namba 11/2022, Luvinga amesema Mfalme Zumaridi na wenzake wanane wanadaiwa kufanya shambulio la kudhuru mwili askari wa Jeshi la Polisi waliofika nyumbani kwake kutekeleza wajibu wao kinyume cha kifungu namba 241 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Washtakiwa hao pia wanadaiwa kuwazuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao kinyume cha kifungu namba 114(A) kifungu kidogo B cha Kanuni ya Adhabu.


Katika kesi namba 12/2022, mwendesha mashataka huyo ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Monica Ndyekubora kuwa Zumaridi na wenzake 92 wanadaiwa kufanya kusanyiko lisilo halali kinyume cha kifungu cha 74(1) na 75 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Washatkiwa walikana mashtaka hayo katika shauri namba 11 na 12 huku upande wa Jamhuri ukiieleza Mahakama kuwa upelelezi kuhusu mashauri hayo mawili umekamilika na kuomba kupagiwa siku ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Kuhusu shauri namba 10 la usafirishaji haramu wa binadamu linalomkabili Mfalme Zumaridi, mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Licha ya mashtaka namba 11 na 12 kuwa na dhamana huku baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamejitokeza kuwadhamini, washtaki wote wanaowakilishwa na Wakili Erick Mutta walikataa dhamana wakisisitiza kuwa wako tayari kwenda mahabusu kuungana na kiongozi wao anayekabiliwa na kesi ya usafirishaji haramu wa binadamu isiyo na dhamana.

Kutokana na uamuzi huo, Hakimu Ndyekubora ameamuru washtakiwa wote kupelekwa mahabusu hadi Machi 17, shauri hilo litakapotakwa kwa ajili ya washatakiwa kusomewa maelezo ya awali katika shauri namba 11 na 12.