Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 4:02 pm

NEWS: MEMBE ATEULIWA KUWA MSHAURI MKUU WA ACT WAZALENDO

Dar es salaam. Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe amemteuwa rasmi hii leo Agosti 3, 2020 aliyekuwa waziri wa Mambo ya njee wa Tanzania, Bernard Membe kuwa Mshauri Mkuu wa Chama hicho.

Membe ameziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa serekali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ambaye kwasasa amekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa.

Katika taarifa iliyotolewa hii leo Agosti 3, 2020 na chama hicho imeeleza kuwa uteuzi wa Nguli huyo wa siasa nchini Tanzania umefanyika chini ya Ibara ya 85(1) inayompa mamlaka kiongozi mkuu wa chama hicho kufanya uteuzi huo.

Uteuzi huo umebarikiwa baada ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya ACTwazalendo Kuridhia kuteuliwa kwake kuwa Mshauri Mkuu wa Chama hii leo katika kikao kinachoendelea katika Ukumbi wa Hotel ya Lamada Jana na leo.

Julai 6, mwaka huu bwana Membe alirejesha kadi ya uanachama wa Chama cha CCM na Julai 15 akatangaza rasmi kujiunga na chama cha ACT Walendo.

Mwanadiplomasia huyo nguli wa zamani alirudisha kadi ya uanachama ingawa Chama cha Mapinduzi kilidai kuwa kilishamfukuza uanachama .

Membe alidai kuwa taratibu za kichama hazikufuatwa, na hivyo bado alikuwa mwanachama halali wa CCM.

Kwasasa Bwana Membe atakuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo baada ya kuombwa na viongozi na wanachama waandamizi wa chama hicho kuchukua fomu ya Urais.

Tuhuma dhidi ya Membe ndani ya CCM

Membe alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kukiuka maadili pamoja na viongozi wengine waandamizi wawili makatibu wakuu wa zamani Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana, ambao wao hawajafukuzwa.

Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole alidai kuwa mwenendo wa Membe ulikuwa si wa kuridhisha toka mwaka 2014.

"Kamati Kuu imeazimia kwa kauli moja kwamba Bernard Membe afukuzwe uanachama wa CCM. Uamuzi huu umekuja baada ya kuwa taarifa zake ndani ya chama zinaonesha mwenendo wake kutoka mwaka 2014 ambako katika chama amewahi kupata adhabu nyingine ambazo zingeweza kumsaidia kujirekebisha," alieleza Polepole.

Membe alikuwa akituhumiwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho kuwa anajipanga 'kumhujumu' Magufuli katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Membe alikuwa akihusishwa kwa muda mrefu na mipango ya kutaka kugombea tiketi ya urais kupitia CCM mwaka huu, hatua ambayo baadhi waliitafsiri kama usaliti.

Japo katiba ya CCM inaruhusu hilo, imekuwa ni ada ya chama kumuachia rais aliye madarakani kupita bila kupingwa kwa awamu ya pili ya urais.


Imeandikwa na Mwandishi Issa H. Deyssa

Imehaririwa na Merry Mgawe.

Hii leo Agosti 3, 2020.

Muakilishi Publisher.