Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 7:09 pm

NEWS: MCHEZAJI WA MAN CITY AVAMIWA NA MAJAMBAZI

Beki wa kulia wa Manchester City Joao Cancelo ameeeleza tukio la kusikitisha la kuvamiwa na majambazi wanne nyumbani kwake na kufanikiwa kumjeruhiwa usoni.

Cancelo, mwenye umri wa miaka 27, alijeruhiwa usoni baada ya kujaribu kupambana na kundi la wezi hao waliovamia nyumbani kwake mwezi Disemba.

"Familia yangu haistahili kupitia ilichokipitia," alisema nyota huyo wa kimataifa wa Ureno, akizungumza na vyombo va habari kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo.

"Ni maisha, inatokea kwenye maisha. Napaswa kusonga mbele."

Cancelo aliweza kucheza katika mcheo ambao City walishinda 2-1 dhidi ya Arsenal mnamo 1 Januari - siku mbili baada ya tukio hilo. Alipimwa na jopo la matabibu na kuonekana anaweza kucheza mchezo huo.

Aliweka kwenye mtandaoni wa Instagram picha kuonyesha majeraha yake saa chache tu baada ya tukio hilo la kutisha.

"Kwa bahati mbaya leo nilivamiwa na watu wanne ambao waliniumiza na kujaribu kuumiza familia yangu," aliandika.

"Unapoonyesha upinzani, ndivyo inavyotokea. Walifanikiwa kuchukua vito vyangu vyote na kuniacha na uso wangu na hali hii."