- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE MUSUKUMA ATAKA MGURUGEZI KUCHUNGUZWA KWA UBADHIRIFU
Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Kasheku maarufu Musukuma ameitaka Serekali kutuma tume ya uchunguzi kumchunguza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kufuatia halmashauri hiyo kufanya manunuzi ya magari ya thamani likiwemo Gari la Mkurugenzi Toyota V8 lenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 400 ambapo amedai manunuzi hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
Musukuma ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Waadishi wa habari Mkoani Geita ambapo amedai mchakato wa manunuzi haujapewa baraka na vikao vya Baraza la madiwani katika Halmashauri hiyo na ni kwenda kinyume na matumizi ya fedha za SCR zinazotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita GGML.
Na ameenda mbali zaidi na kuiomba Serikali kutuma tume ya Uchunguzi kwenye halmashauri hiyo ili kubaini kama mchakato huo ulifuata hatua za kisheria.